Acts 10:1-6

Kornelio Amwita Petro

1 aKatika mji wa Kaisaria palikuwa na mtu jina lake Kornelio, ambaye alikuwa jemadari wa kile kilichojulikana kama kikosi cha Kiitalia. 2 bYeye alikuwa mcha Mungu pamoja na wote wa nyumbani mwake. Aliwapa watu sadaka nyingi na kumwomba Mungu daima. 3 cSiku moja alasiri, yapata saa tisa, aliona maono waziwazi, malaika wa Mungu akimjia na kumwambia, “Kornelio!”

4 dKornelio akamkazia macho kwa hofu akasema, “Kuna nini, Bwana?”

Malaika akamwambia, “Sala zako na sadaka zako kwa maskini zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.
5 eSasa tuma watu waende Yafa wakamwite mtu mmoja jina lake Simoni aitwaye Petro. 6 fYeye anaishi na Simoni mtengenezaji ngozi ambaye nyumba yake iko kando ya bahari.”

Copyright information for SwhKC